
Uraibu wa pombe tishio la ajira za vijana
Dar es Salaam. Wakati pombe ikitajwa kama moja ya vichocheo vya maradhi yasiyoambukiza, athari zake kwa baadhi ya waajiriwa ni kubwa, wakijikuta wanapoteza ajira. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matumizi ya pombe kupita kiasi huathiri uwezo wa kufanya uamuzi, kupunguza umakini na kuharibu afya ya akili, hali inayoweza kutafsiriwa moja kwa moja kama tishio…