
UCHAMBUZI WA MJEMA: Chuki hizi mitandaoni zinatuma ujumbe gani kama taifa?
Ninahuzunishwa na kusikitishwa sana na kile kinachoendelea katika mitandao ya Kijamii hapa Tanzania kwa baadhi ya Watanzania kufurahia madhila yanayowapata wenzetu ikiwamo kifo, jambo ambalo tunapaswa kulitafakari kama taifa. Haya yanayoendelea mitandaoni siyo ya kupuuza hata kidogo kwa sababu huko ndiko mijadala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi imehamia na tusisahau kuwa huko ndiko Watanzania walio…