
Rasmi Samatta kuicheza Le Havre Ufaransa
Nyota wa soka wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Le Havre inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), hatua inayoweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza katika ligi hiyo ya juu nchini humo. Le Havre wamemtambulisha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, wakithibitisha kuwa atavaa jezi namba 70…