
Mpina anukia ACT Wazalendo, kinachomsubiri…
Dar es Salaam. Ukurasa mpya wa siasa za mbunge wa zamani wa Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina unatajwa kufungukia katika Chama cha ACT- Wazalendo, huku akihusishwa na nia ya kuwania urais kupitia jukwaa hilo jipya. Mwanasiasa huyo amewawakilisha wananchi wa Kisesa kwa miongo miwili tangu mwaka 2005 kwa nafasi ya ubunge, kabla ya jina…