
Mganga aliyebaka akidai anafanya tambiko akwaa kisiki mahakamani
Arusha. Usemi wa Kiswahili usemao “Mganga hajigangi” umethitika baada ya mganga wa kienyeji kutoka mkoani Geita, Masoud Adam ambaye alijikuta akikosa pa kujitetea baada ya Mahakama ya Rufani kukataa rufaa aliyoiwasilisha kupinga kifungo cha miaka 30 jela alichohukumiwa kwa kosa la ubakaji. Katika kesi ya msingi iliyosikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Masoud alishtakiwa…