Josiah aziingiza vitani mbili Bara
Namungo na Dodoma Jiji zimeingia vitani kuisaka saini ya aliyekuwa kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Aman Josiah, lakini inadaiwa itakayokuwa na mkwanja mnene inaweza ikafanikisha dili hilo kwani kwa sasa kocha huyo hana timu. Chanzo cha ndani kutoka Namungo kilisema uongozi umeshawishika kutaka huduma ya Josiah kutokana na kile alichokifanya akiwa na Prisons msimu uliyopita,…