
Mawakili, TLS wataka askari aliyemsukuma Lissu kushughulikiwa
Dar es Salaam. Mawakili wa Tundu Lissu, ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wamelaani kitendo cha askari wa Jeshi la Magereza kumsukuma mteja wao mahakamani. Wameiomba Mahakama na Jeshi la Magereza kuchukua hatua kuzuia vitendo vinavyofanywa na askari hao. Tukio linalolalamikiwa lilitokea Julai 30, 2025 baada ya kuahirishwa kesi ya uhaini inayomkabili Lissu katika Mahakama ya…