
Asilimia 17 ya umeme unaozalishwa nchini unatumika Dar
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Jiji hilo linatumia megawati 678 za umeme uliopo kwenye gridi ya Taifa kiwango ambacho ni sawa na asilimia 16.8 ya umeme wote uliokuwa unazalishwa hadi Aprili mwaka huu. Kwa sasa mahitaji ya juu ya umeme katika Gridi ya Taifa nchini yameendelea kuongezeka…