
WAKULIMA WAPEWA ELIMU KUHUSU MBEGU ZINAZOSTAHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI
Ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, wakulima na wadau wa kilimo wametakiwa kutopitiliza bila kutembelea mabanda ya Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula (TFSRP) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Katika mabanda haya, wakulima wanapata fursa ya kujionea mbegu mpya za mazao zilizozinduliwa mwaka huu…