Bado Watatu – 7 | Mwanaspoti
“MUME wako anaitwa nani?” “Anaitwa Omar Kikasha.” “Hakuna mtu mwingine anayeishi katika nyumba hii anayetumia jina hili?” Nilianza kutomuamini mwanamke huyo kwa kuhisi alikuwa anatuficha. Tabia ya binaadamu akishaona mtu anaulizwa na polisi hata kama hajui amefanya kosa au la, anamficha. Sijui ni kwanini? “Mume wako yuko wapi?” nikamuuliza. “Anafanya kazi wapi?” “Mume wangu ni…