
Watumishi majumbani wapaza sauti kilio cha haki
Dodoma. Wafanyakazi wa majumbani wamepaza sauti wakitaka kupewa haki zao za msingi za likizo ya mwaka, ugonjwa na ya uzazi kama ilivyo kwa kada nyingine za kazi nchini. Vilevile wanataka haki ya kuwa na muda maalumu wa kufanya kazi na kupumzika kwa kuwa waajiri wengi hawatoi nafasi kwao ya kupumzika, hivyo hujikuta wakifanya kazi zaidi…