
Jamii Yakumbushwa Kutowatenga Wenye Kifafa: “Kifafa Sio Laana Wala Mkosi”
TAASISI ya Tanzania Epilepsy Organisation (TEO) imeitaka jamii kuwapa heshima, upendo, na haki sawa watu wenye ugonjwa wa kifafa, ikisisitiza kuwa hawapaswi kutengwa wala kunyanyapaliwa. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025 wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wa Ongea, Simama Imara, Suzana Mukoyi, aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, amesema mradi huo umeanzishwa…