
Majaliwa: Rushwa bado tishio nchi za SADC
Arusha. Licha ya maendeleo katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), rushwa inatajwa kuwa tishio la usalama linalosababisha uhalifu uliopangwa, biashara haramu ya binadamu, ugaidi na mmomonyoko wa utawala wa sheria. Hayo yamesemwa leo Jumatatu Agosti 4, 2025 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan,…