Watiania ubunge, uwakilishi Chaumma kujulikana kesho
Arusha. Zikiwa zimesalia siku nne kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kufanya uteuzi wa watiania wa nafasi za urais, ubunge na udiwani, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kinatarajia kupitisha majina ya wagombea wake kesho, Agosti 24, 2025, baada ya kikao chake kilichoanza leo. Vyama vya siasa nchini vinaendelea na mchakamchaka wa kuwateua…