
Mafuriko yaua watu watatu, yaacha zaidi ya 100 bila makazi
Kampala. Watu watatu wamefariki dunia huku zaidi ya watu 100 wakipoteza makazi baada ya mafuriko makubwa kuyakumba maeneo ya Mbale na Sironko nchini Uganda. Taarifa iliyotolewa na tovuti ya habari ya Daily Monitor ya Uganda imeeleza kuwa mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha tangu Jumapili, Agosti 17, 2025, na kusababisha uharibifu wa miundombinu…