
VIDEO: Simulizi za wanawake Handeni na maswahibu utafutaji kuni, ugumu kutumia nishati safi
Tanga. “Tunakutana na nyoka na wadudu wengine hatari, tunachomwa na miba na visiki,” anasimulia Mashabani Mchelo, mkazi wa Handeni Mjini, mkoa wa Tanga. Anasema safari ya kwenda porini kutafuta kuni huchukua kati ya saa mbili hadi tatu kwenda na kurudi, na mara nyingine zaidi ya hapo kutokana na ugumu wa upatikanaji wa kuni. Mashabani, anayeishi…