DUA MAALUM KWA TAIFA ,RAIS SAMIA YAFANA DAR

Anaripoti Rashid Mtagaluka

Tukio la Dua ya kuiombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan lililofanyika leo Agosti 31,2025 katika ukumbi wa DRIMP, Ilala Boma, ni kielelezo cha namna Watanzania wanavyotambua dhamana kubwa aliyoibeba Rais katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Dua hiyo iliyoongozwa na Sheikh Adam Mwinyipingu wa BAKWATA Ilala, imekusanya makundi mbalimbali ya kijamii wanawake, wanaume, vijana kwa wazee, ikiwa ni alama ya mshikikano na mshikamano wa kitaifa.

Kinachovutia zaidi ni kwamba tukio hili limeandaliwa na mwanadada jasiri na mwandishi wa habari anayeheshimika, Fatma Jalala, kupitia taasisi yake ya Seed of Changes.

Hii ni ishara kwamba vijana, hususan wanawake, wanajitokeza mbele sio tu kama wachambuzi wa habari, bali pia kama wabunifu wa matukio yenye tija kubwa kwa taifa.

Licha ya changamoto za kiutekelezaji, Fatma hakusita kuchukua jukumu la kuandaa tukio kubwa la kuliombea taifa na kiongozi wake mkuu jambo linaloonyesha uthubutu, uzalendo na imani ya dhati katika uongozi wa Rais Samia.

Katika kuliombea taifa, Dkt. Samia na viongozi wengine wote wa vyama 18 vyenye wagombea waliotia nia.

Aidha dua hiyo iliyojulikana kwa jina la Munajjat ya Samia na Taifa ilibeba Kauli mbiu inayosema, ” Bila Amani hakuna ndoto inayotimia”

Ujumbe ambao umebeba dhamira ya dhati ya kuwasisitiza Watanzania kuwa na wivu mkubwa na amani waliyonayo, hivyo wailinde na kuzidi kumuomba Mungu ajaalie amani na utulivu uliopo nchini udumu.

Kwa upande wa Rais Samia, dua hii ni ujumbe mzito kwamba wananchi wanaomwona kama dira ya matumaini, kiongozi anayebeba maono ya mshikamo na maendeleo ya Watanzania wote.

Ni heshima na upendo wa wananchi kwa kiongozi wao, wakimuombea apate nguvu, ulinzi na ujasiri wa kukabiliana na vikwazo vinavyoweza kuibuka katika safari ya kuelekea uchaguzi.

Kwa hakika, tukio hili linapaswa kuwa somo kwa vijana wengine nchini: kwamba mabadiliko na mafanikio makubwa hayahitaji kusubiri misaada ya nje, bali uthubutu, dhamira na moyo wa kujitolea kwa ajili ya taifa.