……….
JESHI la Polisi limewataka watu wote wanaomiliki silaha haramu kinyume na sheria kuzisalimisha kwa hiyari kunzia Sepetemba 01, hadi Oktoba 31, mwaka huu ambao ndiyo muda wa msamaha ulitolewa na Serikali.
Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo David Misime, alisema hayo leo jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msamaha wa kutoshitakiwa kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria.
“Msamaha huo ni kwa wahusika kutoshitakiwa endapo watasalimisha silaha hizo haramu kwa hiyari na kwa muda uliopagwa. Hivyo kulingana na tangazo la Serikali Na. 537, la Agosti 29,2025 wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria wanapaswa kusizalimisha kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa,”alisema
Alisema, usalimishaji wa silaha haramu kwa hiyari nchi nzima utafanyika siku yoyote kuanzia Sepetemba 01 hadi Oktoba 31, 2025.
“Silaha haramu zisalimishwe katika kituo chochote cha polisi nchini, Ofisi ya Serikali za Mitaa au kwa Mtendaji Kata/Sheia kuanzia muda wa saa 02:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni,”alisema
Aidha, alisema mtu yeyote atakaye salimisha silaha haramu ndani ya kipindi hicho hatachukuliwa hatua zozote za kisheria.
“Mtu atakayepatikana na silaha haramu baada ya kipindi cha masamaha atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,”alisema Msime
Kadhalika aliwasisitiza wananchi wote ambao ndugu zao walikuwa wanamiliki silha kihalali na wamefariki wahakikishe wanazisalimisha kuingana na masharti yaliyotajwa.”
Aidha, wamiliki binafasi wa silaha zikiwemo kampuni binafasi za ulinzi ambazo zimekuwa zikiazimaau kuazimisha silha kwa watu wengine waache tabia hiyo mara moja kwani ni kosa la jinai na kama kuna silha ambazo zinatumika isivyo halali zirejeshwe kwa wamiliki au zisalimishwe katika vituo vya polisi katika kipindi cha msamaha ulitolewa na Serikali,”alisema
Misime, alisema msamaha huo ni moja ya juhudi na mikakati inayotekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa mikataba, itifaki maazimio na makubaliano mbalimbali ya kuzuia uzaagaji wa silaha ndogo na nyepesi.
“Moja ya maazimio ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa ni yale yaliyofanyika mwezi julai 2018 kuhusu udhibiti wa uzagaaji wa silaha haramu duniani kwani umekuwa ukisababisha uvunjifu wa amani, ukosefu wa usalama , hofu kwa watu, vifo na majeruhi