Watu 1,000 wamefariki dunia huku mmoja akiokolewa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliotokea katika eneo la Darfur nchini Sudan.
Maafa hayo yanatokea wakati Taifa hilo lkingia mwaka wa tatu wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliopekekea vifo vya maelfu ya watu na hali ngumu ya maisha na ukosefu wa usalama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi la waasi la The Sudan Liberation Movement/Army wanaokalia mji huo, imeelezwa kuwa Maporomoko hayo yalianzia katika eneo la milima ya Marra magharibi mwa Sudan kisha kabla ya kufunika Kijiji cha Tarasin.
Baada ya mvua kubwa iliyonyeesha mfululuzo katika eneo hilo lenye kambi za wakimbizi waliopata hifadhi ya muda.
Wamesema maporomoko hayo ya udongo yaliharibu kijiji kizima katika eneo hilo lililop Darfur magharibi mwa Sudan.
“Taarifa za awali zinaonyesha vifo vya wakazi wote wa kijiji, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watu elfu moja, na mtu mmoja tu alinusurika,” imeelezwa,.
Waasi hao pia wameomba msaada kwa UN ili kukoa miili kutoka kwenye kiiji hicho kilichofunikwa na maporomoko hayo.
Pia walitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada ya kimataifa kwa usaidizi wa kurejesha miili ya waathirika, ambayo ni pamoja na watoto.
Hata hivyo, makundi ya vuguvugu na Jeshi la Ukombozi la Sudan, ambalo linadhibiti eneo hilo limeahidi, kuendelea kupigana pamoja na jeshi la serikali halali ya Sudan.
Licha ya changamoto zinazowakabili wakazi wa eneo hilo ambao wengi ni wakimbizi wa mapigano baina ya jeshi la Sudan na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) waliopo katika Jimbo la Darfur Kaskazini wakibiluwa na uhaba mkubwa wa chakula na dawa.
Elidaima Mangela kwa msaada wa Mashirika ya habari