TAKUKURU Kinondoni Ilivyofuatilia Miradi ya Bilioni Moja – Global Publishers

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa TAKUKURU Kinondoni, Christian Nyakizee.

Dar es Salaam, 2 Septemba 2025: Taarifa iliyowasilishwa leo na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa TAKUKURU Kinondoni, Christian Nyakizee inahusu mafanikio katika utendaji kazi wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni kwa kipindi cha Aprili mpaka Juni 2025 ambapo taasisi hiyo imetekeleza majukumu ya kufuatilia miradi ya maendeleo, kuendesha program ya TAKUKURU Rafiki, kutoa elimu kwa umma na kufanya uchunguzi kwa tuhuma mbalimbali kama ifuatavyo.

1.UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

“Kama mnavyofahamu katika jitihada za kuzui vitendo vya rushwa Takukuru inalo jukumu la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa inatekelezwa kwa ufanisi lakini pia thamani ya fedha katika miradi hiyo inaonekana.

“Katika kutekeleza jukumu hili TAKUKURU ilifuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo minne yenye thamani ya zaidi ya bilioni moja (1,080, 383,481.93) na katika miradi hiyo miradi miwili katika sekta ya afya ilibainika kuwa na mapungufu yafuatayo.

“.Mradi wa ujenzi wa jengo la magonjwa ya mlipuko katika Zahanati ya Kijitonyama wenye thamani ya Tsh. 150,000,000.00. ulikutwa na mapungufu kwenye gharama za ujenzi wa jengo hilo kukisiwa kuwa kubwa kuliko uhalisia wa jengo.

“.Mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji na wadi ya wazazi katika Zahanati ya Mpiji Magohe Manispaa ya Ubungo, mradi huu ulikutwa na mapungufu kwenye madirisha 6 ya aluminum hayakuwa yamefungwa raba vizuri (seals) hivyo kupelekea vioo kuvunjika au maji kupenya nyakati za mvua. Amesema Nyakizee na kuendelea kusema.

BAADA YA KUBAINI HAYO HATUA ZIFUATAZO ZILICHUKULIWA

“.Kuanzisha uchunguzi ili kuthibitsha thamani ya fedha kwenye mradi huo.

“.Kuitisha kikao na wadau ambao ni Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, na kukubaliana kufanya marekebishao kwa mapungufu yaliyobainika ikiwemo kuhakikisha raba (seals) za kwenye madirisha zifungwe vizuri.

KAZI NYINGINE ZILIZOFANYIKA

2.Elimu kwa umma

“Katika kipindi hiki tuliendelea na jukumu la uelimishaji umma kwa kuendesha semina 23, mikutano ya hadhara 20, maonesho 7, vipindi vya redio 5, Uandishi wa Makala 3, na kuhimarishwa kwa klabu 28, za wapinga rushwa mashuleni na vyuoni.

ELIMU IMESAIDIA YAFUATAYO

“i.Ufanisi wa usimamizi wa miradi ya maendeleo umeongezeka.

ii.Wananchi wamehamasika kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.

iii.Kupungua kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa katika ngazi ya mitaa, vijiji na kata.

TAKUKURU RAFIKI

“Utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU Rafiki uliendelea kwa kufanya vikao 12 katika kata 12 na kero 40 zilizoibuliwa zilitatuliwa kuputia vikao vya mrejesho.

“Kupitia Programu hii tuliweza kurewjesha viti 10 vya kukalia wageni kutoka ofisi ya kata ya Tandale vilivyokuwa havijulikani vilipoenda na viti hivyo kurejeshwa kwa viongozi wa kata hiyo.

UCHUNGUZI NA MASHITAKA

“Malalamiko 120 yalipokelewa katika kipindi hicho ambapo malalamiko 76 yalihusu vitendo vya rushwa na malalamiko 44 hayakuhusu vitendo vya rushwa.

“Malalamiko 76 yalihusu vitendo vya rushwa ambapo uchunguzi wake bado unaendelea ukiiwa katika hatua mbalimbali.

“Malalamiko 44 ambayo hayakuhusu rushwa walalamikaji walishauriwa.

“Katika kipindi tajwa kesi 27 zinaendelea mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 6 ni mpya ambazo zilifunguliwana kesi 3 Jamhuri ilishinda.

MIKAKATI YA TAKUKURU MKOA WA KINONDONI KWA KIPINDI CHA JULAI MPAKA SEPTEMBA 2025

Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu madhara ya rushwa na umuhimu wa ushiriki wao katika vitendo vya kuzuia rushwa haswa tynapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

WITO

Wananchi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa njia zifuatazo:

i.Kufika ofisi za TAKUKURU mkoa wa Kinondoni na Wilaya za Ubungo.

ii.Kupiga simu ya bure 113 au simu ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni 0738150236

Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Ubungo 0738150238. Alimaliza kusema Nyakizee katika ripoti hiyo.