Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KABLA ya kwenda mbali na kukumalizia bandle lako nataka nikwambie tu huu ni mwaka Uchaguzi Mkuu ikifika Oktoba 29,2025 tunaenda KUTIKI kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Ndio hivyo unakunja sura itakusaidia nini? kunjua sura ndungu yangu maisha yenyewe ndio haya haya. Sawa tufanye hutaki kumpa kura yako Rais Samia unampigia nani kwa jinsi unavyoona?.
Usijichoshe ukifika kwenye karatasi ya kupiga kura nenda moja kwa moja katika picha ya Rais Samia weka tiki tena ikae vizuri ,kisha angalia aliko mgombea mwenza wake Dk.Emmanuel Nchimbi nako weka TIKI.
Kwa wabunge na madiwani huko sasa utaamua, maana watakuja kuomba kura wasikilizeni lakini kwa nafasi ya Urais tunaenda na Rais Samia tu.
Wote tunafahamu tuko katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu hivyo mengi yatasemwa, mengi yatasikika lakini baada ya kusikiliza wagombea wote basi kumbuka Rais ni Dk.Samia tu,hakuna mwingine.
Katika miaka minne na nusu ambayo ametuongoza Watanzania tumeridhishwa na utendaji kazi wake, tumeridhishwa na jinsi alivyosimamia maendeleo ya Watanzania katika maeneo mbalimbali.
Hakuna cha kumlipa zaidi ya kumpigia kura ashinde kwa kishindo. Hana baya mama wa watu, Mungu amempa moyo wa subira, moyo wa upendo na kubwa zaidi amejaaliwa unyenyekevu wa kutosha.
Rais Samia anaongoza nchi kwa kutumia falsafa yake ya R4 ambazo ndani yake kuna Maridhiano, Ustahimilivu, Kujenga upya na Mabdiliko, hivyo katika uongozi wake Rais Samia ametuongoza kwa kutanguliza R4, na hakika falsafa hiyo nchi yetu imekuwa salama salimini.
Uongozi wake umekuwa tofauti na huko nyuma na sina sababu ya kuelezea maana mzee wetu wa Serikali ya Awamu ya pili mzee Rais Ali Hassan Mwinyi (Hayati) aliwahi kueleza kıla zama na kitabu chake na kama ndio hivyo basi kitabu cha zama za Rais Dk.Samia kinabeba uongozi wenye upendo, unyenyekevu dhidi ya anaowaongoza.
Katika uongozi wa Rais Samia ametufundidha maana halısı ya kiongozi kuwa mlezi kwa anawaongoza .Hakika tunajivunia Urais wa Dk.Samia Suluhu Hassan na kwa jinsi ambavyo ametuongoza sina shaka hata kidogo kura za Watanzania zote zinaelekezwa kwake.
Najua wagombea wengine wa nafasi ya Urais watapita kunadi Ilani zao lakini ndugu zangu tuzungumze ukweli hivi kuna mpinzani mwenye Ilani inayoidizi Ilani ya CCM?,atoke wapi kwa mfano!
Acha ushamba wewe Ilani ni ya CCM tu ile ambayo Rais Samia anakwenda kuitekeleza. Wakati anazindua kampeni zake pale Kawe jijini Dar es Salaam aliweka bayana mambo ya msingi yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030.
Wote tuliyasikia sina sababu ya kurudia .Tusichoshane kwani wakati anazungumza ulikuwa wapi? Wee vipi!! Hata hivyo Rais Samia wakati wa uzinduzi wa kampeni zake alieleza kuna mambo muhimu ambayo ataanza nayo katika siku 100 za kwanza baada ya kuunda Serikali yake.
Kuna mambo 13 muhimu lakini kwa sababu ya muda nitaje mambo matatu atakayofanya ndani ya Siku 100 za mwanzo.Rais Samia anasema ataanza kwa majaribio mfumo wa Bima ya afya kwa wote ambao utagusa wajawazito, wazee na watoto. Yaani hapa watapata bima ya afya kwa fedha za Serikali.
Huyo ndio Rais Samia anayesubiri kura yangu kikubwa tuombe uzima tu. Jambo lingine ambalo atalifanya katika siku 100 za mwanzo ni kugharamia vipimo vya moyo, figo na sukari.
Hilo ni jambo kubwa na ukweli linakwenda kutatua changamoto ambazo Watanzania wanakumbana nazo katika kutafuta fedha za kujitibu katika magonjwa hayo. Jambo lingine ambalo Rais Samia atalifanya ni kutoa ajira 12,000 zitakazogusa sekta ya elimu na afya.
Lengo ni kuhakikisha wananchi anaowaongoza wanakuwa na uhakika wa matibabu ya afya… Hapo sijazungumzia ile ahadi ya Rais kwamba atapiga marufuku hospitali zote nchini kutoza fedha miili ya marehemu.
Nani ambaye hajui hii kitu ilivyokuwa inaongeza uchungu kwa ndugu wa marehemu… Wapo baadhi ya watu waliogopa kufuata miili ya wapendwa wao maana wanatamani kuzika lakini wakiangalia deni wanaogopa kufuata mwili.
Rais Dk.Samia kwa upendo wake mkubwa kwetu ameamua katıka siku 100 za mwanzo anakwenda kupiga marufuku.Tunaposema kura yetu ni kwa Rais Samia muwe mnaelewa basi.Acheni kujitoa ufahamu.
Katika akili ya kawaida tu wakati Rais Samia anaeleza mambo makubwa kwa ajili ya Watanzania huko upande wa pili wa upinzani kuna mmoja ya wagombea anakuja na sera ya kupiga marufuku kitanda cha sita kwa sita eti kiwe futi nne.
Lakini pia wanaokunywa pombe wawe wanapewa leseni.Hayo ndio mawazo ya baadhi ya wagombea wa urais wa upinzani tulionao mawazo yao ndio yalipokomea.Wale wengine wao ndio wanaendelea kukomaa na ile No Reform No Election .
Na kıbaya zaidi wakakosa şifa kwa sababu tu ya kutojaza fomu ya maadili ya Uchaguzi mkuu. Misimamo mengine ni ya hovyo sana .Kwanza shauri yao , sisi tunakwenda na Dk.Samia wengine waendelee kuweka mpira kwapani.
Hata hivyo wakati naisubiria kwa hamu Oktoba 29 kwenda kumpigia kura Rais Samia ngoja nikwambie mtu wangu hivi umesikia habari ya kule Mbagala katika usafiri wa mwendo kasi, ndugu zetu wameanza kutumia mabasi yenye kiyoyozi.
Hakuna tena mambo ya kufungua vioo na lile joto letu kwenye daladala hadi unasikia harufu ya kikwapa inaenda kumalizika. Yaani hivi sasa unasafiri kwenye basi ambayo ndani full kipupwe unategemea nini?
Ni raha tu na wale waliokuwa wanashindwa kugombania daladala sasa ni mwendo wa kupanga foleni unaingia katika basi kwa raha mustarehe. Wale wa Gongolamboto nao wanasubiria kwa hamu maana Ujenzi wa barabara ya mwendo kasi ni kama vile wako mwishoni kumalizia.
Mbona Mbagala watainjoi lakini ukweli ili kuwa na uhakika wa miradi ya mwendo kasi na miradi mingine ya maendeleo kura yako hakikisha inakwenda kwa Rais Samia,kazi ameiweza na sasa ni wakati wetu kumpa zawadi ya thamani ambayo ni kumpigia kura.
Hata hivyo sitaki kuzungumza sababu za kwanini mitano tena kwa Rais Samia maana hizo zimeshazungumzwa vya kutosha na wote tunajua .Kwani utekelezaji wa miradi mikubwa hujaona?kwa wale wanaotumia treni ya SGR Dar -Dom wanaijua vizuri kazi ya Samia, na hao siku zote wanasema wako pamoja na Dk.Samia.
Hapo ujue sijazungumzia kabisa kwenye sekta ya michezo,timu za mpira siku hizi wanaogelea fedha tu .Siunajua kuna GOLI LA MAMA. Lakini hapo sizungumzii kabisa ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya michezo mbalimbali.
Naamini kabisa wana michezo hasa wapenda soka tayari wanajua kura yap inakwenda kwanani? Ni kwa Samia tu. Katika nishati safi ya kupikia huko ndio mama Samia kafanya maajabu makubwa, kuni na mkaa sasa imebakia kuwa historia katika maeneo mengi.
Siku hizi mwanamke dakika tano tu ugali au wali uko mezani. Ugomvi wa chakula kinaiva saa ngapi haupo tena siku hizi na Rais Samia ameshasema kazi ya kuhamasisha nishati safi iko pale pale.
Baba lishe na Mama lishe najua mnafahamu kura yenu ya Urais ni kwa Mama Samia tu,mama kinara wa nishati safi Afrika. Kwa urais ni kwa Mama Samia.
Bodaboda ninyi ndio sina cha kuwaambia maana serikali inayoongozwa na Rais Samia imekuwa na urafiki mkubwa na ninyi na wenyewe mnajua ,hata yale mambo ya kamatakamata yamepungua.Siku hizi sio shida zenu.
Lakini hata trafiki mnajua namna ya kumalizana nao halafu upendo wa Rais Samia kwa bodaboda hata faini kwa wale wanaokiuka sheria ni elfu 10, tu ile ya elfu 30 waachiwe wenye magari.
Kwa leo inatosha,Rais Samia amefanya mengi makubwa na yamegusa maisha ya Watanzania kila mahali.Ugomvi wa wakulima na wagugaji umeisha siku hizi na kama upo ni ule tu ambao unazungungumzika.
Ahsante Rais Samia na binafsi nasema kwa sasa ni wewe tu 2025-2030.Ndio tushaamua,halafu ile nyomi ya kwenye mikutano yake acha kabisa,ni hatari faya kwa sauti ya Piere Liquid.
TUKUTANE OKTOBA 29 ,KURA KWA DK.SAMIA SULUHU HASSAN
ALIYEKWAMBIA SİNA
SIMU NANI -0713833822.