MKAKAMU WA RAIS AWEIKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA KUTIBU SARATANI

…………..

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango

amesema
Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za tiba za kitalii,
ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha na kuimarisha sekta ya afya nchini na
kuchangia kwenye Pato la Taifa.

 

Makamu wa
Rais amesema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kituo
cha Mafunzo na Matibabu ya Saratani pamoja na kuzindua Kituo cha Upandikizaji
Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. Amesema m
chango wa Utalii wa Tiba kwenye Pato la Taifa kwa sasa unakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 166.5 ambapo idadi wa wagonjwa wanaokuja
kutibiwa nchini imeongezeka kutoka 5,700 mwaka 2021 hadi 12,180 mwaka 2025
.

 

Makamu wa Rais ametambua mchango
wa Hospitali ya Benjamin Mkapa
kwa Utalii Tiba,
unaotokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Miundombinu, Vifaa
tiba vyenye teknolojia ya kisasa na Wataalamu waliobobea katika maeneo
mbalimbali.
Amesema hatua
hi
yo inatoa fursa ya
kuendelea kupanua huduma za Utalii Tiba zitakazowezesha wagonjwa kutoka nchi
mbalimbali
kuja kwa wingi kutibiwa
nchini.

 

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Hospitali
ya Benjamin Mkapa kwa ubia na Sekta Binafsi au Halmashauri ya Jiji
kuangalia uwezekano wa kujenga jengo maalum kwa ajili ya
huduma za malazi na nyinginezo kama chakula na fedha, kwa ndugu na
wagonjwa wanaotoka nchi Jirani au mikoani, hususan pale wanaposubiri matibabu
au kuruhusiwa kurejea makwao baada ya matibabu.

 

Aidha, Makamu
wa Rais ametoa rai
kwa
Wizara ya Afya, Madaktari na Wahudumu wote wa afya,
kuhakikisha kuwa elimu kwa umma kuhusu
kujikinga na magonjwa inahusisha Shule, Vyuo, Taasisi za Kidini, NGOs, na
Taasisi za Kijamii ili kuongeza jitihada katika kuwakinga Watanzania na
magonjwa ya kuambukiza na hata yasiyoambukiza, ili kuepuka gharama kubwa za
matibabu.
Amewasisitiza kuwa wabunifu
katika kutoa elimu
kwa kutumia njia
mbalimbali na hasa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na mifumo ya
kidigitali ili kuwafikishia wananchi elimu hiyo muhimu
.

 

Pia Makamu wa Rais ameilekeza Wizara
ya Afya kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Serikali
Mtandao kuhakikisha mifumo
ya matibabu katika Hospitali za kitaifa na zile
maalum za kikanda
inasomana ili kurahisisha
mwendelezo wa matibabu
.

 

Vilevile, Makamu
wa Rais ametoa wito kwa
Wizara ya Afya kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha kuweka utaratibu wa kuwasomesha na kuwaendeleza
madaktari hadi kufikia ngazi ya
ubingwa na ubobevu katika
kutibu magonjwa ya saratani, upandikizaji wa figo na upandikizaji wa uboho. Amesisitiza
umuhimu wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuangalia uwezekano wa kuanzisha ushirikiano na
wataalam wengine kutoka nje ya nchi kama vile Japan, Korea na mataifa mengine
ili kuwajengea wataalamu wa nchini uwezo na kubadilishana uzoefu. Amesema
katika kuandaa Madaktari bingwa na bobezi itafaa mafunzo yao yatolewe sambamba
na ya wataalam wengine husika, mfano mafunzo ya Daktari wa figo yaende pamoja
na mafunzo ya wataalam wa damu, maabara, wauguzi, mionzi, na chakula na lishe.

 

Makamu wa Rais amewasihi Madaktari na Wahudumu
wote wa afya katika Hospitali
ya Benjamin Mkapa na
Hospitali zote nchini
kuzingatia kiapo cha maadili ya taaluma yao, kujituma na kutoa huduma zenye viwango na
zinazomjali mgonjwa.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif
Shekalaghe amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa katika sekta afya
ikiwemo uboreshaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, wananchi kutoka mataifa
mbalimbali Jirani wameendelea kupata matibabu katika Hospitali za hapa nchini.

 

Amesema Serikali ya Awamu wa Sita imeimarisha huduma
za afya kuanzia katika zahanati hadi hospitali za kibingwa kwa kuzingatia ilani
ya uchaguzi kama ilivyoahidi kwa wananchi.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin
Mkapa amesema katika kipindi cha miaka kumi ya hospitali hiyo, kumepatikana
mafanikio makubwa ikiwemo kuanzishwa kwa huduma za ubingwa wa juukama vile
matibabu ya magonjwa ya figo, upandikizaji wa uloto,matibabu ya magonjwa ya
moyo, maabara maalum ya kuzibua mishipa ya damu, upasuaji wa mishipa ya fahamu
na ubongo, kubadilisha nyionga na magoti, matibabu ya homoni pamoja na matibabu
ya watoto wachanga.

Ametaja mafanikio mengine ikiwemo kuendesha mtambo wa
kuzalisha hewa ya oksijeni wenye uuwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa siku,
uwepo wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi, kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa
wa juu karibu na wananchi kupitia huduma mkoba na tembezi pamoja na kufanya
tafiti za tiba kwa kushirikiana na taasisi zingine.

Katika hafla hiyo, Serikali imepokea rasmi mradi wa kimkakati wa Kituo cha Umahiri
cha Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Upandikizaji Uloto na Sayansi ya Magonjwa
ya Damu kitakachojengwa hapa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma. Inatarajiwa kuwa mradi huu utakapokamilika
utatatua changamoto ya matibabu ya upandikizaji uloto, katika hadhi ya ubingwa bobezi
kwa kutoa huduma ambazo hazipatikani katika ukanda wa Afrika Mashariki.