Bado Watatu – 18


Jioni ya siku ile nikakutana na Hamisa katika hoteli ya Mtendele. Nilimpigia simu na kumjulisha kuwa tukutane hapo saa moja usiku. Kutoka siku hiyo ndopo tukawa mapenzini na Hamisa. Hamisa alifanikiwa kuharibu akili yangu nikawa kama zezeta. Kwa kuona nilikuwa polisi alinieleza mkasa wake ambao ninataka kukuhadithia kwa vile una fundisho ndani yake.