Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 4, amewasili wilayani Mbalizi, mkoa wa Mbeya, na kupokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi.
Wananchi wakiwa na nyuso za furaha, nyimbo na nderemo walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Mlima Reli kumlaki na kumsikiliza kiongozi huyo anayeendelea na mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Ziara hii ni sehemu ya muendelezo wa kampeni zake za kitaifa, ambapo Rais Dkt. Samia anaendelea kuwasilisha Ilani ya CCM na kueleza dira ya maendeleo ya miaka mitano ijayo kwa wananchi wa Mbeya na maeneo jirani.