RAIS DK.SAMIA KUWAPA ZAWADI YA TAA ZA BARABARANI VIJANA JIJINI MBEYA ILI WAFANYE BIASHARA SAA 24

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mbeya 

MGOMBEA Urais kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwapa zawadi ya taa za barabarani wananchi wa Jiji la Mbeya ili vijana waweze kufanya biashara saa 24.

Dk.Samia ameyasema hayo leo Septemba 4,2025 alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya Mjini akiwa katika mkutano wake wa kampeni kwa ajili ya kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

“Mbeya imekuwa kibiashara na miundombinu tunajenga , vijana wengi wako Mbeya wanajiajiri kwa maana hiyo nataka niwape zawadi ndogo pamoja na yale yaliyoahidiwa kwenye Ilani mimi kama mgombea nitakapopata ridhaa yenu nitaweka taa za barabarani.

“İli vijana wafanye kazı saa zote na mataa ya ili vijana waweze kujiari kwa saa 24 tunajua tukiweka taa biashara zitashamiri na mtajiajiri hiyo ndio zawadi yangu kwenu.

“Kuna miradi naifikiria kuifanya lakini haiko kwenye Ilani na hii sio ahadi.Huwa napita pale Mwanjela taa zinavyowaka na watu wanavyopata shida kuvuka barabara hivyo nafikiria kujenga daraja ka kuvusha watu.

“Nilikuwa nafikiria hivyo sasa hii ikiwezekana ila Mataa ni ahadi yangu nitawaambia Wizara waie kuweka hili lingine ikiwezekana,”amesema Dk.Samia huku akitumia nafasi hiyo kuomba kuomba kura ambapo Oktoba 29 wananchi waende kumchagua Rais,wabunge na madiwani wote wa CCM ndani ya Mkoa wa Mbeya.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema kuna barabara zimeelezwa hivyo amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuwa wanakwenda kujenga na lengo la Serikali ni kuuunganisha Wilaya zote na Makao makuu ya Mkoa nchini kote.

Akizungumza kuhusu kilimo amesema ndani ya Mkoa wa Mbeya baada ya kuhamasisha kilimo kwa Kiasi  kikubwa na baada ya kuleta umeme sasahivi wamemaliza  vijiji vyote na wanakwenda kwenye vitongoji kumaliza vyote.

Ameongeza kuwa kwa sasa kinachofuata ni kuweka Kongani za Viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa ndani ya Mkoa wa Mbeya yasafirishwe yakiwa yameongezwa thamani.“Kwahiyo tunakwenda kuanzisha kongani za Viwanda na Mbeya nayo inakwenda kupata kongani hizo”