ZAIDI YA 1000 KUHUDHURIA MKUTANO WA NYAMA YA NGURUWE DAR

ZAIDI ya wajumbe 1,250 wa kimataifa na ndani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa sekta ya nguruwe barani Afrika unaotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Septemba 11 hadi 13, mwaka 

Mkutano huo utafanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, kuzungumzia  hatua muhimu kwa sekta ya ufugaji wa nguruwe inayokuwa kwa kasi nchini.

Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wafugaji wa Nguruwe Tanzania (TAPIFA) utawakutanisha wafugaji wa nguruwe, wafanyabiashara, watafiti, watunga sera na wawekezaji kutoka barani yote.

Akizungumza jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TAPIFA, Doreen Maro amesema takriban nchi tisa za Afrika tayari zimethibitisha kushiriki, huku wajumbe 250 wakitarajiwa kutoka nje ya Tanzania ambapo  kwa jumla, si chini ya watu 10,000 wanaotarajiwa kushiriki, ana kwa ana na mtandaoni.

“Hii ni fursa nzuri kwa Watanzania kujifunza, kuchunguza na kuwekeza katika sekta ambayo inakua kwa kasi lakini bado haijathaminiwa,” amesema  Maro.

“Ufugaji wa nguruwe sio tena shughuli ya mashambani. Unakuwa mhusika mkuu katika usalama wa chakula wa kitaifa na ukuaji wa uchumi.” 

Ameongeza.

TAPIFA, ambayo inawakilisha wafugaji wa nguruwe wadogo na wakubwa nchini ilisajiliwa rasmi mwaka 2016 na kuanza kazi mwaka 2017. Chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wafugaji, upatikanaji wa soko, na uboreshaji wa teknolojia ya ufugaji na ulishaji.

Kulingana na Maro, wafugaji wa nguruwe nchini wanakabiliwa na changamoto kuu, ikiwa ni pamoja na uhaba mkubwa wa vichinjio vilivyoidhinishwa. Vifaa vilivyopo mara nyingi huwanyonya wakulima kwa kuchukua viungo vya ndani vya thamani na kuwaacha na nyama ndogo tu.

“Wakulima wanapungukiwa. Tunahitaji kanuni na uwekezaji unaowalinda na kuhakikisha wanapata thamani kwa kazi yao ngumu,”