
Bado Watatu – 19 | Mwanaspoti
“NITAKWENDA.”“Basi nitakuja twende sote.”“Sawa. Nitakusubiri.” Saa nane mchana Raisa akaja nyumbani. Nikakaa naye hadi saa tisa tulipoondoka kwenda Hospitali ya Bombo iliyoko eneo la Raskazoni pembezoni mwa Bahari ya Hindi.Ukiwa hospitalini hapo unaweza kuiona bahari na bandari ya Tanga. Tulipofika hospitalini hapo, muda wa kutazama wagonjwa ulikuwa umewadia. Tukaingia ndani na kufika katika wodi aliyokuwa…