DB Lioness Vs Polisi Stars hapatoshi

Timu ya DB Lioness ilitinga nusu fainali ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), baada ya kuifunga timu ya ngumu ya Polisi Stars kwa michezo 2-1.

Robo fainali hiyo iliyohudhuriwa na watazamaji wengi, ilifanyika kwenye Uwanja Donbosco, Oysterbay.

Kwa matokeo hayo, timu ya DB Lioness itacheza na Jeshi Stars katika nusu fainali, ambayo nayo  ilitinga hatua hiyo, baada ya kuifunga Pazi Queens katika michezo 2-0.

Katika robo fainali ya tatu, ilichochangia kwa maafande wa Jeshi Polisi Stars kupoteza mchezo huo, ilionyesha ni kutokana kuchelewa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Donbosco, Oysterbay.

Kwa upande wa timu ya DB Lioness iliyofika mapema,  kwa lengo la kuuzoea uwanja huo uliofanyiwa ukarabati, ilisaidia timu hiyo kupata ushindi

 Katika robo fainali ya kwanza DB Lioness ilishinda kwa pointi 93-70, robo fainali ya pili Polisi Stars ikashinda kwa pointi 65-73, na robo fainali ya tatu DB Lioness ikashinda kwa pointi 69-49.

Kwa upande wa timu ya Polisi Stars walionyesha uwezo mkubwa   ni Irene Kapambala, Faidha Ismaili, Jacquelyn Masinde na Merina Remy.

Upande wa timu ya DB Lioness, alikuwa Taudencia Katumbi, Gloria Mbeta na Lavender Orondo.