::::::
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema hakuna Hakuna uvamizi uliofanyika katika ofisi za Jamii Forums na Kilichotokea ni utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Serikali na wadau wake.
Kupitia ukurasa wa mitandao ya kijamii wa msemaji huyo ameandika kuwa “Hakuna uvamizi uliofanyika katika ofisi za Jamii Forums. Kilichotokea ni utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Serikali na wadau wake ambapo leo Maafisa wa Serikali walikwenda kuwasilisha barua ya wito kwa Jamii Forums. Ndugu Maxence Melo usilete taharuki isiyo na sababu za msingi, toa ushirikiano”
.