Kikao cha 19 cha Kamati ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kimefanyika Mkoani Arusha katika ukumbi wa VETA-Njiro kikihusisha wajumbe kutoka taasisi mbalimbali.
Kikao hicho kimekusudia kujadili maendeleo ya mifuko na programu za uwezeshaji hapa nchini ikiwemo inayotoa mikopo, dhamana, ruzuku pamoja na programu mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Washiriki wa kikao hiki ni wajumbe wote wa kamati hiyo, waratibu wa mifuko na programu za uwezeshaji pamoja na wataalam wa TEHAMA.
Katika kikao hicho, wajumbe walipata pia fursa ya kuona Mfumo Jumuishi wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji (National Empowerment Management Information System – NEMIS).