MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA SULUHU HASSAN AKISALIMIANA NA KUOMBA KURA KWA WANANCHI JIMBO LA UYOLE

Na Said Mwishehe,Mbeya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan akisalimiana Wananchi wa Jimbo la Uyole Mkoani Mbeya waliofurika Barabarani kumlaki wakati wa Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu leo September 05,2025.

Dk.Samia wamepata nafasi ya kusalimiana na wananchi hao na kisha kuomba kura akiwa njiani akielekea wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni ya kuomba kura ambako Septemba 4 aliingia Mkoa huo akitolea Mkoa wa Songwe ambako amefanya mikutano katika majimbo mbalimbali ya Mkoa huo.