Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mgombea urais, Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuanzisha kongani za viwanda mkoani Mbeya ili kuongeza thamani ya mazao, kuzalisha ajira na kuinua kipato cha vijana.
Akiwa Mbeya Mjini Septemba 4, 2025, Samia pia ameahidi kujenga daraja Mwanjelwa, kuweka taa za barabarani Ilomba, Meta na Uyole–Kyela, pamoja na kuendeleza ruzuku za pembejeo za kilimo.
Aidha, amesema serikali itakamilisha machinjio ya kisasa Utengule, kusajili na kuchanja mifugo yote kwa ajili ya soko la nyama la nje, na kuhakikisha huduma za uzazi zinajumuishwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wasio na uwezo.
Related