WADAU WA MAENDELEO WAASWA KUJITOKEZA KUFANYA UWEKEZAJI WA NDANI.

Wadau mbalimbali wa maendeleo wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali hususani katika sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini.

Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani mbogwe mkoani Geita, umefanikiwa kutembelea na kuweka jiwe la msingi katika kituo binafsi cha afya cha Kagala kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya mbogwe.

Kituo cha afya Kagala kimegharimu takribani kiasi cha sh bilioni tatu ambapo kitaenda kupunguza msongamano kwenye vituo vya afya vya maeneo ya karibu.

Kiongozi wa mbio za mwenge 2025 Ismail Ali Ussi amewataka wawekezaji wengine kujitokeza kufanya uwekezaji ili kupanua huduma mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha afya cha Kagala Bunga Dadu amesema kuwa mradi huo umelenga kutoa huduma bora ya afya, kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja na kupunguza adha ya kufata huduma mbali.