BENDERA ZA CHADEMA ZIKIPEPEA KWA MADAHA KUFURAHIA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS CCM…

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Njombe

KUNA mambo yanaleta raha Kiasi kwamba hata wale ambao hawana nafasi ya kuzungumza basi hutumia mbinu mbalimbali kufikisha ujumbe kwa jamii inayozunguka

Leo Septemba 6,2025 wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) ukifanyika katika Jimbo la Makambako mkooni Njombe pamoja na kuwepo na mabango mbalimbali yaliyokuwa yakinoesha mkutano huo.

Hata hivyo pamoja na kuwepo picha za mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan,mabango yenye picha mgombea ubunge Jimbo la Makambako Daniel Chongolo,uwepo wa kapu la mama lenye maneno yaliyoandikwa mitano tena pia kulikuwa na bendera za CCM ambazo zilikuwa zimefungwa katika milingoti iiliyopachikwq juu ya miti katika eneo la mkutano huo.

Mbali ya bendera za CCM pia kulikuwa na bendera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambazo zilikuwa sehemu moja na zile bendera za CCM.

Hata hivyo bendera zote hasa za CHADEMA zilikuwa zinapepea bila kuchoka yaani upepo ulivyoongezeka ndivyo ambavyo nazo zilivyozidi kupepea,si unajua bendera hufuata upepo na ndio ilivyo kwa bendera za CHADEMA ambazo nazo zilionekana kufuata upepo na kama ni upepo wa kisiasa basi habari ya mjini ni kampeni za CCM na mgombea wake Urais Dk.Samia ambaye kila anakokwenda maelfu ya wananchi wamekuwa wakitokeza kutokana na kufurahia kazi nzuri ya Dk.Samia na Oktoba mwaka huu wanakwenda KUTIKI.

Hata hivyo wakati bendera za CHADEMA zikipepeq tena kwa mbwembwe akili iliyonijia ni ile kauli mbiu yao ya No Referm No Election yaani wakati viongozi wa CHADEMA wakisimamoa kauli mbiu lakini pia kukosa şifa ya kushiriki uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa upande wa bendera zao zenyewe hazina habari kabisa.

Yaani bendera za CHADEMA zilizonekanq katika mkutano huo zilikuwa zinafuraha ya kushuhudia mkutano huo uliofanyika Jimbo la Makambako ambalo mgombea wa Jimbo hilo ni Daniel Chongolo ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM.