DK.SAMIA SULUHU HASSAN AIHIMIZA MAKUNDI YAVUNJWE CCM İLİ KUWA WAMOJA“ TUSIISHIWE POWER”

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mafinga

MWENYEKIITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho katika Uchaguzi mkuu mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wana CCM kuvunja makundi na iwawe wamoja ili wasiishie Power kama walivyo wengine.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za Urais kuelekea Oktoba 29,2025 uliofanyika Mafinga Mkoani Iringa Dk.Samia amesema katıka mchakato wa kura za maoni kwa ajili ya wagombea ulishamalizika.

“Natambua katika uchaguzi kwa ajili ya wahombea wetu ndani ya Chama ulishamalizika na wakati ule wakati wa kugombea makundi yalikuwa mengi ,waombeaji walikuwa wengi lakini ulifanyia uteuzi.Nataka kuwaambia wana Mafinga walioteuliwa Mungu amependa iwe hivyo na ambao hawakuteuliwa wasubiri wakati mwingine

“Niwaambe sana sana tuvunje makundi na sio Mafinga  peke yake ni majimbo yote ya uchaguzi ndani ya mkoa wa Iringa ili tuende kwenye uchaguzi tukiwa wamoja na chama kiwe na nguvu kisiishie Power kama walivyoishia wengine.Twende tukiwa na nguvu kama Chama kimoja cha CCM.”

Wakati huo akizungumza katika mkutano wa Mafinga kabla ya kumkaribisha Rais Dk.Samia kuzungumza na wananchi .Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Kenani Kikongosi ametumia mikutano ya kampeni za Chama hicho kuwaaambia vijana wasiandamane na badala yake waandamane katika kutafuta fedha.

“Kumekuwa na tabia ya watu kuwahamasisha vijana kwenda kufanya vurugu lakini waende kwenye maandamano yasiyorasmi ya uvunjifu wa amani.Andamaneni  kutafuta fedha, andamaneni kulima, andamaneni kufanya biashara.

“Andamaneni kufanyabiashara ambazo zitawaingizia kupato ninyi pamoja na familia zenu.Msiende kuandamana kwa masilahi ya watu binafsi ambao familia zao hazipo ndani ya taifa letu, wao wanako kwa kukimbilia wewe huna pa kukimbilia.”