Mechi za mtego Kagame hizi hapa

MICHUANO ya Kombe la Kagame inatarajiwa kuendelea tena kesho, Jumapili, kwa mechi mbili kupigwa ambapo Madani itakabiliana na Al-Hilal Omdurman huku Mogadishu City ikipambana na Kator katika mechi zinazotarajiwa kuamua mwelekeo wa kundi C.

Katika mechi zao za kwanza katika mashindano hayo yanayohusisha klabu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hakuna timu iliyoibuka na ushindi, jambo linaloongeza presha kwa mechi za leo zitakazochezwa kwenye uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Madani ililazimishwa suluhu na Kator ya Sudan Kusini huku Al-Hilal Omdurman ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mogadishu City ya Somalia. Matokeo hayo yalitoa picha ya ushindani uliopo kundi hilo.

Madani na Al-Hilal Omdurman ambazo zitacheza mechi ya mapema, ni timu ambazo zinafahamiana vizuri kutokana na wote kutoka Sudan, hivyo itakuwa mechi yenye ushindani kutokana na rekodi zao.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Julai 10, 2025 hakuna mababe ambaye alipatakana walitoka suluhu. Ukirudi nyuma katika michezo mitano iliyopita, Al-Hilal Omdurman imeshinda mitatu na kutoa sare mbili.

Hivyo Madani itakuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Al-Hilal Omdurman kwani tangu wakutane kwa mara ya kwanza 2012 hawajawahi kuifunga miamba hiyo ya soka la Sudan, ushindi wao huwa sare.

Kwa upande wa Mogadishu City, sare ya bao 1-1 dhidi ya Al-Hilal Omdurman imeacha shauku ya kupata ushindi wa kwanza kutokana na kiwango kizuri ilichoonyesha kwenye mechi hiyo.

Timu hii ina wachezaji wenye kasi na uwezo wa kushambulia haraka, kitu ambacho kiliwapa wakati mgumu Al-Hilal Omdurman katika mechi ya kwanza. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana katika mashindano yote.

Mechi hizi leo zitaamua mwelekeo wa kundi C, kwani hakuna timu iliyoshinda kwenye mzunguko wa kwanza. Pointi tatu za leo ni muhimu kwa kila kikosi ili kuondoa mzigo wa sare.

yo, akisaidia Ethiopian Coffee kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Garde Cotes ya Burundi katika mechi ya Kundi A iliyopigwa Ijumaa kwenye uwanja wa KMC.

“Nimefurahi sana kwa mchezo mzuri tuliouonyesha na mabao mengi tuliofungwa. Hii inatupa motisha kuelekea mechezo wetu wa mwisho wa kundi dhidi ya Kenya Police,” alisema mshambuliaji huyo.

Admassu alifunga hat-trick hiyo katika dakika ya 37, 45+2 na 57, mabao mengine ya Ethiopian Coffee katika mechi hiyo yalifungwa na Abubakar Adamu na Zelalem Abate ambaye alifunga mawili.

Kwa upande wake. kocha wa Ethiopian Coffee, Abiy Kassahun alieleza umuhimu wa ushindi huo.

“Tunapaswa kuendelea kuwa makini, lakini timu ni wazi kuwa timu imenifurahisha kwa kiwango cha mchezo leo. Mabao haya yatatupa nguvu ya kuendelea na mchezo wetu ujao,” alisema.

Kwa matokeo hayo, Ethiopian Coffee ndio kinara wa kundi A ikiwa na pointi nne sawa na Singida BS, Polisi inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu huku Garde Cotes ikiburuza mkia.