Mtemvu azindua kampeni za Zungu Ilala

MWENYEKITI WA Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abass Mtemvu,amesema wamejipanga vyema kuhakikisha MgombeaUrais Dk.Samia Sukuhu Hassan anapata kura za kishindo mkoani humo.

Ameyasema alipokuwa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu alipo zindua kampeni za CCM katika jimbo la Ilala,Dar es Salaam, Jana.

Mtemvu alisema Rais DK. Samia, amefanya mambo makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeo mkoani humo hivyo wananchi wana wajibu wa kumejeshea shukrani Kwa kura za kishindo.

Alieleza katika mkoa huo Rais Dk. Samia, ametekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata.

“Nina mwombea kura Rais Dk.Samia, wagombea ubunge wa majimbo yote na wagombea udiwani wa kata zote za Mkoa wa Dar es Salaam,” alieleza Mtemvu.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala,Zungu alisema anaimani kubwa na gombea urais CCM Rais Dk. Samia kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

“ Kila mwanachama wa CCM siku ya kupiga kura aende na mpenzi wake, ndugu yake au mtoto wake. Akienda na watu watatu tu basi Rais Samia Dk. Samia, atapata kura milioni 39. Atakuwa ameshinda kwa ki atapata kura milioni 39. Na huu utakuwa ni ushindi wa kishindo,”alieleza Zungu.

Pia, alisema anaimani kubwa uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu utakuwa, huru na wa haki.

“Tanzania ni nchi yenye utawala bora ya kwanza Afrika. Nchi yenye amani na upendo. Haya yana letwa na Mwenyezi Mungu na amempa upendo mkubwa Rais Dk. Samia wa kutupenda sisi watoto wake katika taifa lake,”alibainisha Zungu.

Alisema, agenda za mgombea urais wa CCM Dk. Samia, zimejikita kuleta kasi kubwa ya maendeleo katika siku 100 za kwanza za uongozi wake.

“Taifa letu tumeweka utu na amani mbele. Hataka kama uko chama kingine mpe kura Rais Dk. Samia ambaye ameshika dira ya taifa letu,”alieleza Zungu.

Awali Mwenyekiti WA CCM Wilaya ya Ilala, Said Side,alisema, mpaka sasa kata nane katika ya 36 za wilaya hiyo wabasubiri kura za ndiyo na hapana kutokana na kutokuwa na wagombea wa vyama vya upinzani.

Alisema hali hiyo atatokana utekelezaji wa kiwango wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25.

“Hivyo Oktoba 29 mwaka huu CCM katika Wilaya ya Ilala, tutapata ushindi wa kishindo katika majimbo yote manne,ambayo ni Ilala, Ukonga,Segerea na Kivukoni,”alisema Sidde.