DK NCHIMBI AWAHUTUBIA WANANCHI WA JIMBO LA KWELA,SUMBAWANGA VIJIJINI.

MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Kwela katika Uwanja wa Laela A,Sumbawanga Vijijini katika mkutano mdogo wa hadhara wa Kampeni leo Jumatatu Septemba 8,2025.

Baada ya kuwahutubia Wananchi,Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo pia kuwanadi wagombea Ubunge wa Mkoa wa Rukwa akiwemo Mbunge wa jimbo la Kwela,Deus Clement Sangu pamoja na Madiwani.

Dk.Nchimbi ameingia Mkoani Rukwa leo kuendelea na mikutano yake ya kampeni ya kutafuta kura za kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.