Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewashukuru wananchi wa jimbo la Kalambo kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa kuomba kura za mgombea Urais kupitia Chama hicho Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Akitokea jimbo la Kwela,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Dkt.Nchimbi amewashukuru Wananchi wa Jimbo la Kalambo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wake wa hadhara wa kampeni
Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano wake wa hadhara,Balozi Dkt.Nchimbi aliwanadi wagombea Ubunge wa mkoa wa Rukwa akiwemo Mbunge wa jimbo la Kalambo,Edifonsi Joackim Kanon pamoja na Madiwani.
Dk.Nchimbi ameingia Mkoani Rukwa leo kuendelea kusaka kura za kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.