Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema timu ya Gor Mahia kutoka Kenya ambayo itacheza mechi ya kirafiki kwenye kilele cha wiki ya Simba Day itawasili usiku wa leo hapa nchini.
Leo Simba ilitembelea na kutoa msaada katika Kituo cha Kutunza Watoto Wenye Uhitaji cha Twarika Kadiliya kilichopo Mabibo, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ahamed amesema timu hiyo itawasili leo na kesho kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi hiyo.
Ameongeza kuwa baadhi ya wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu ya taifa watakapomaliza majukumu watajumuika na wenzao kwa ajili ya tamasha hilo.
“Wachezaji walioko timu ya taifa, hasa wale wa Tanzania, baada ya mechi watapanda ndege na kuungana na wenzao. Ni tamasha ambalo maandalizi yake kwa asilimia kubwa yanakwenda vizuri,” amesema Ahmaed.