Dodoma. Hatima ya kugombea urais kwa Luhaga Mpina kupitia Chama cha ACT -Wazalendo sasa imebaki mikononi mwa majaji kwa siku tatu zijazo baada ya kesi hiyo kupangwa kusikiliza Septemba 11, mwaka huu.
Leo Jumatatu Septemba 8,2025 katika Mahakama Kuu Masijala Kuu- Dodoma, Mpina na mgombea mwenza wake Fatuma Fereji wameshiriki kesi hiyo iliyokuwa mbele ya jopo la majaji watatu, Abdi Kagomba, Evaristo Longopa na John Kahyoza na mawakili watatu kutoka kila upande.
Mpina alienguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Endelea kufuatilia taarifa zaidi katika mitandao yetu