…………….
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mchinga mkoa wa Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), . Salma Rashid Kikwete, amezindua rasmi kampeni zake jana 7 septemba,2025, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Uzinduzi huo umefanyika katika kata ya Rutamba Manispaa ya Lindi na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, wakiongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa