Global TV Yatangaza Nafasi za Watangazaji – Global Publishers



Kampuni ya utangazaji ya Global TV imetangaza nafasi za kazi kwa vijana wenye vipaji na shauku ya kujiunga katika timu yake ya vipindi vya runinga.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa, jumla ya nafasi 6 zimefunguliwa:

🎤 Burudani & Udaku – nafasi 4

🎤 Masuala ya Kijamii – nafasi 2

Miongoni mwa sifa zinazohitajika ni kuwa mkazi wa Dar es Salaam, kuwa tayari kufanya internship, kuwa na vyeti vya kitaaluma pamoja na kuwa mbunifu, mwenye bidii na shauku kubwa ya kazi ya utangazaji.

Aidha, tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni Septemba 15, 2025, na waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja katika ofisi za Global TV zilizopo Mori Road, Sinza – Dar es Salaam, au kwa mawasiliano kupitia namba 0687 531 251.

Kwa mujibu wa Global TV, lengo la nafasi hizi ni kuwapa vijana wenye vipaji fursa ya kukuza taaluma zao katika tasnia ya habari na burudani.