Baba’ke Kamwe ndani kwa Mkapa Simba Day

BABA mzazi wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe yupo kwa Mkapa akishuhudia kilele cha wiki ya Simba Day.

Mzee Shaaban Kamwe ambaye amekuwa akitangaza kuwa ni shabiki wa Simba ameingia uwanjani akikaa jukwaa la VIP.

Mzazi huyo wa msemaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ameingia uwanjani tangu saa 10:00 jioni akiwa na mtoto wake mwingine amevalia uzi mpya wa Simba, kofia na kitambaa alichokiweka shingoni.

Mbali na kukaa katika jukwaa hilo, lakini Mzee Kamwe anaonekana kufurahia shoo ya mwanamuziki Mbosso aliyeingia jukwaani kupafomu tangu saa 11:02 jioni akiimba ngoma kama Kunguru, Ova Sijakaa Sawa, Selemani na nyinginezo ambazo zimeibua shangwe.

Tangu mtoto wake aanze kazi Jangwani mwaka 2022 mzazi huyo amekuwa maarufu mitandaoni kutokana na upinzani wa Simba na Yanga, lakini pia yeye na mwanawe wanaoshabikia timu mbili zenye upinzani wa jadi Tanzania.