ACHANA na mauzo ya jezi, biashara inayoonekana kuuzika kwa kiasi kikubwa ni vyakula mbalimbali.
Ukiwatoa wale wanaouza kwenye mabanda hatua chache kidogo na Uwanja wa Mkapa, kuna walioweka meza pembezoni mwa uwanja huo uliowekewa uzuo.
Kila aina ya chakula unayoijua ipo kwa Mkapa siyo chipsi na vitu vingine wala wali na ugali zipo sambusa zile za nyama na viazi.
Nyama choma pia zipo ziel za ngo’mbe na mbuzi, ndizi za kukaanga na kuchoma na pia kuna watu mbalimbali wale waliovalia jezi za Simba na wengine wapo wanaopata huduma hiyo.
Mmoja wa wauza vyakula ameiambia Mwanaspoti kuwa kutokana na msongamano wa watu ameongeza bei ya chipsi kuku akiuzwa Sh4,000 badala ya 3,500.
“Nilichukua magunia mawili ya viazi na nimeanza kuuza tangu saa sita mchana, kuna watu wengi hivyo nikaona niongeze bei,” amesema.