Chino aingia na staili ya zombi 

MSANII wa Bongo Fleva na dansa maarufu, Chino Wanaman ndiye msanii wa kwanza kuburudisha kilele cha wiki ya Simba Day akiingia na staili ya zombi.

Leo ni kilele cha Simba Day ambacho baadaye kitahitimishwa na burudani ya soka, Simba ikiialika Gor Mahia kutoka Kenya.

Msanii huyo ameingia kusherehesha kwa Mkapa akiongozana na msanii wa singeli, Dogo Sajenti ambaye amekuwa akimsimamia.

Zaidi ya madansa 20 ameingia nao uwanjani nyota huyo wa kibao cha Tiririka akiongozana na vijana zaidi ya 10 waliojichora sura zao kama mazombi.

Mbali na burudani anayotoa Chino, lakini vijana hao 10 walikuwa na shoo ya kipekee wakiburudisha majukwaa tofauti.