Dkt. Samia Awaomba Wananchi Kujitokeza kwa Wingi Oktoba 29 – Video – Global Publishers



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025, ili kukiwezesha CCM kupata ushindi wa heshima na kishindo.

Dkt. Samia alitoa wito huo Septemba 10, 2025, alipohutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika wilayani Igunga, mkoani Tabora.

Akihamasisha kura, Dkt. Samia alisema ushindi wa kishindo siyo tu utathibitisha uimara wa CCM, bali pia utaziba midomo ya wapinzani na kuonesha mshikamano wa wananchi kwa chama hicho.

“Mtakapokuja na ushindi wa heshima  kwa jina jingine ushindi wa kishindo wa CCM  tutaweza kuziba midomo ya wale wengine. Lakini pia inapendeza sana kuona wana