Mafuriko ya watu mahakamani Mpina akipigania haki yake

Dodoma. Idadi ya watu waliofika mahakamani leo kusikiliza kesi ya mgombea urais wa Chama cha ACT –Wazalendo, Luhaga Mpina imeongezeka ukilinganisha na siku zingine.

Watu wengi waliofika mahakamani leo wamevalia nguo zinazotumiwa na chama hicho kama sare yao ingawa wengi wanaonekana kuwa na nguo za kawaida na wote wameruhusiwa kuingia katika ukumbi wa Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma, ambapo hukumu ya kesi hiyo itasomwa.

Kesi ya Mpina inahusu kupinga kuenguliwa katika mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Agosti 27,2025 ilimzuia kuingia ndani ya jengo ili akabidhi fomu zake na kuteuliwa.

Majaji watatu Abdi Kagomba, Evaristo Longopa na John Kahyoza ndiyo wanasubiriwa kutoa hatima ya mustakabali wa ama Mpina atagombea au kukosa kabisa fursa hiyo.

Tofauti na wakati mwingine, leo maofisa wa Mahakama hiyo jumuishi walijipanga kuwapokea na kuwapa maelekezo wananchi waliofika na hata ukumbi ulipojaa watu wengine walielekezwa kukaa katika ukumbi wa pili, ambako pia wangeweza kufuatilia kila kitakachoendelea ukumbi inaposomwa hukumu ya kesi hiyo.
 

Kingine kilichovutia leo wakati Mpina akiingia mahakamani ni kitendo cha machifu ambao walikuwa wamemzunguka na hata alipokaa alikaa nao wawili, mmoja kila upande.
Mmoja wa machifu alibeba usinga na mwingine alikuwa na kirungu ambacho aliomba abaki nacho pale Polisi walipoomba akikabidhi