MAKATIBU WAKUU WA MALIASILI NA UTALII EAC WAKUTANA ARUSHA.

……………………..

Na Sixmund Begashe, Arusha 

Makatibu wakuu wanaoshughulikia Maliasili na Utalii Afrika Mashariki wamekutana Jijini Arusha kwa lengo la kukamilisha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mawaziri wa sekta hiyo kutoka nchini zinazo unda Jumuhia ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 12  Septemba 2025 Jijini Arusha

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini, baada ya kikao hicho kilichojumuisha wataalam wa Uhifadhi kutoka nchi za Jumuhia hiyo,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Uhifadhi Kamishna wa Polisi Benedict, Wakulyamba amesema maandalizi yote yameenda vizuri. 

CP. Wakulyamba ameongeza kuwa, kikao hicho ni muhimu kwa ustawi wa uhifadhi wa Maliasili na Utalii kwa kuwa utaendelea kuimarisha uwelewa wa pamoja wa Uhifadhi endelevu wa Maliasili na Utalii.

Aidha amewapongeza Maafisa na  wataalam wa uhifadhi hapa nchini kwa kushiri kikamilifu katika maandalizi ya kikao hicho hasa kwa kutanguliza uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.