MGOMBEA URAIS UDP KUIPATIA CHATO MKOA MPYA

Mgombea urais kupitia chama cha UDP, Saum Rashid, akiomba kura kwa wananchi wa wilaya ya Chato.

Wananchi wakiendelea kusikiliza sera za mgombea urais kupitia chama cha UDP

……………

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha United Democratic party (UDP), Saum Rashid, ameahidi kuipandisha hadhi wilaya ya Chato kuwa mkoa mpya iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Mbali na hilo amesema miongoni mwa sera za UDP ni pamoja na kufufua na kuimalisha viwanda nchini, ikiwemo kiwanda cha kuchambua na kukamua mafuta ya zao la Pamba, kilicho chini ya Chama kikuu cha Ushirika Chato(CCU).

Nikutokana na kiwanda hicho kuwa mkombozi na kimbilio pekee la wakulima wa zao la Pamba katika wilaya ya Chato mkoani Geita na Biharamulo mkoani Kagera,ambapo wananchi walikuwa na uhakika wa kuuza zao hilo kwa bei kubwa.

Alikuwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika stendi ya zamani mjini Chato, huku akisiwasihi wananchi kukichangua UDP iwapo wanahitaji maendeleo ya kweli.

Amesema anatambua kiu kubwa na hitaji la muda mrefu la wananchi wa wilaya ya Chato kupatiwa mkoa, na kwamba anakunbuka hoja hiyo imekuwa ya muda mrefu licha ya serikali ya CCM kuahidi kupitia vigezo vinavyo hitajika ili kuitangaza.

“Naomba mtuamini Chama Cha UDP na mkituchagua kuongoza nchi hii lazima Chato iwe mkoa na nimefika Chato na kuikagua vigezo vyote vipo na mnastahili kupata heshima hiyo” amesema Saum.pp0

Mbali na hilo, amesema Chama hicho kitahakikisha wananchi wote wanapatiwa Bima za afya bure ili kuwa na uhakika wa matibabu kwa wote pasipo kubagua daraja la huduma kwa kuwa Afya ni suala mhimu kwa binadamu yoyote.

Kadhalika UDP itatoa kipaumbele kwa kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi wao kupitia kilimo cha kisasa.

Awali Katibu wa Chama hicho wilaya ya Chato,Amos Lukinda, amesema wananchi wa wilaya hiyo hawana sababu ya kukichangua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu hakuna kinachoweza kujivunia kwa wananchi wa wilaya hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Amewataka wananchi wa wilaya hiyo kukichagua UDP kwa madai kuwa ndiyo Chama pekee cha upinzani kilichokuwa cha kwanza kupata nafasi ya uongozi wa serikali za mitaa wilayani Chato baada ya kuanza rasmi mfumo wa vyama vingi chini.

                            Mwisho.